SITOKUSAHAU.
SEHEMU YA-02.
Tony hakutaka kuongea chochote kwa mama japo alionekana kuwa na jambo mhimu la kuongea.Maongezi ya hapa na pale yaliendelea lakini kubwa zaidi alilolisema mama yake ni kuwa awe makini sana hasa katika suala zima la kimapenzi,
“Dunia ya sasa ukijiingiza kwenye hayo mambo basi ujue utapotea mwanangu jambo ambalo silitaki litokee”Aliongea mama yake ikiwa ni usiku tayari.Lakini Tony alimuondoa wasiwasi na kumwambia kuwa hakuna kitakachoharibika kwa upande wake.Hatimaye ikabaki siku moja ya Tony kusafiri hadi hjadi Moshi ili akaendelee na masomo yake.Mama yake alimuandalia vitu mbali na mbali na kesho yake Tony akapanda basi hadi Moshi.Baada ya kufika kwa mjomba wake aliingia moja kwa moja chumbani kwake akionekana kutafakari mambo mengi kichwani mwake,
“Kweli wamenifanyia hivyo?nauchukia umasikini kupita kiasi”Alijisemea baada ya kutafakari sana hadi machozi yakamtoka akionekana kuwa na masikitiko ya hali ya juu,
“Lakini hakijaharibika kitu wacha nipambane na huku”Alijisemea tena,usingizi ulimpitia.Kesho yake asubuhi alifika chuoni na kama kawaida yake hakutaka hata kuongea na mti yaani hakupenda hata kuwasalimia wanachuo wenzake.Kichwani alionekana kuwa na mambo mengi lakini hayo mambo hayakumzuia yeye kusoma kwa bidii na kujifunza mengi sana.Hakika kichwa chake kilishika mambo mengi tena kwa mda mfupi.
*
Ndani ya chuo hicho kulikuwa na mwanafunzi mmoja aliyeitwa Maria Alex,alikuwa msichana mzuri sana,alipenda kuvaa kiheshima sana,yaani katika wanachuo wote waliokuwa pale basi yeye ndo alivaa nguo ndefu zisizoacha hata mwili wake nje,sketi alihakikisha inafika miguuni.Alikuwa mturivu sana hakupenda maongezi kama ilivyokuwa kwa Tony.Hakika kila kijana alitamani kuwa naye kwani weupe wake wa asili ndo ulimzidishia uzuri,hakuwa na rafiki yeyote Yule,aliishi peke yake.Kila mara Tony alikuwa akimwangalia Maria na kujikuta akitabasamu taratibu moyo wa Tony ukaanza kumpenda Maria,lakini alijitahidi kujizuia huku akiyakumbuka maneno ya mama yake kuwa asijiingize kwenye masuala hayo.Alijitahidi kuuzuia moyo wake lakini hisia hazifichiki.Kadri siku zilivyokuwa zinasogea ndivyo Tony alizidisha upendo kwa Maria,njia za kumwambia zilishindikana na kubaki akiumia moyoni,
“Inamaana kweli maneno ya mama yamenitoka? Ahaahapana ngoja nijizuie”Alijisemea Tony huku akifuta fikra zilizokuwa zimemtawala kichwani.Siku zikasogea huku Maria hali yake ikiwa ni ile ile hata Tony naye ikawa hivyo,
“Kweli hapa chuoni tuna mabubu wawili”Alisikika msichana mmoja akisema akiwazungumzia Tony na Maria.Hata kipindi cha michezo Tony alibaki ndani hakupenda kujichanganya na watu wengine,
“Hahahahaaha Tunu bwana umesahau kuwa jogoo wa shamba hawiki mjini?”
“alafu kweli maana hata anaonekana jinsi alivyo mshamba mavazi hayo hata kanisani kwa sahivi hayavaliwi” Yalikuwa ni maneno ya wasichana wawili wakimjadili Maria,wengi wao walihisi labda ni mtu wa kijijini ndo maana mambo yake yalionekana kuwa ya kijijini kijijini.Hawakujua kuwa Maria alizaliwa Moshi mjini na baba yake alikuwa na utajiri mkubwa sana ambao hakutaka kuuonyesha kwa watu.Baba yake aliitwa Alex,alikuwa na magarimatano huku matatu yakiwa ni ya abiria,mawili yalikuwa ni kwa ajili ya kutembelea.Kwao na Maria walizaliwa watano huku wote wakiwa ni wa kike,kitendo kile kilimchukiza sana Alex kwani alijisemea kuwa kama akifa basi hakutakuwa na mtu wa kurithi mali zake.Licha ya kuwa ni watoto wake lakini aliwachukia sana,alikuwa na maduka matatu hapo hapo Moshi.Kwake kusomesha watoto wa kike aliona kama ni uharibifu wa pesa na ndo maana kati ya watoto wake watano alimsomesha mmoja tu ambaye ni Maria na hapo alimpeleka chuoni hakutaka kumpeleka kwenye shule za gharama akihisi labda ataharibu pesa zake.Maria alijitahidi kusoma kwa bidii lakini mtoto ili afanikiwe lazima mzazi wake amuunge mkono.Alex hakufuatilia hata matokeo ya mwanaye.Maria alikuwa wa mwisho kuzaliwa hivyo dada zake wote waliiishia darasa la saba tu na wote walikuwqa wameolewa tayari.Hivyo nyumbani pale aliishi dada wa kazi pamoja na mke wake Alex,
“Umeoana sasa?kuzaa matoto ya kike yanakuwa sio yako tena angalia sasa yameolewa yote” Alex aliongea kwa hasira mbele ya mke wake,
“Lakini mme wangu tambua kuwa mwenyezi Mungu ndiye mpangaji hivyo hayo mambo tumwachie Mungu” Mke wake alijibu kwa sauti ya chini yenye majonzi ndani yake,
“Mshenzi mkubwa wewe,Mungu ndiye mpaji lakini anasema aombaye hupewa” Alex alimjibu mkewe kwa jazba.Hapo mkewe alinyamaza mara moja kwani kuendelea kubishana na mmewe alitambua fika Alex huwa hana utani.Maisha ya mama yake Maria yakawa ya mashaka sana kwani amani ndani haikuwepo tena,kila kukicha Alex akawa mtu wa kumfokea mama yake Maria.
**MIAKA ISHIRINI NYUMA*
Alex baada ya kuona mke wake anazaaa watoto wa kike tu ndipo aliamua kumtafuta mke wa nje akiamini kuwa anaweza kumzalia mtoto wa kiume.Kwa wakati huo mkewe alikuwa na mimba ya miezi ya miezi miwili.Bahati nzuri akakutana na mwanamke mmoja bila kujua kuwa mke huyo alikuwa na mimba ya mwezi mmoja kwa wakati huo na mimba hiyo ilikuwa ni ya mwalimu wa shule ya sekondari iitwayo St Hamed iliyoko huko huko Moshi.Basi alianza kuishi na Yule mwanamke akamjengea nyumba na kumuachisha kazi ya umamantilie aliyokuwa anaifanya Yule mwanamke.Alimhamishia Moshi mjini na hapo akacha kulala nyumbani kwake akawa analala kwa Yule mwanamke aliyejulikana kwa jina la Amina.Siku zikakatika,
“Baby nina mimba yako” Aliongea Amina akimwambia Alex ikiwa imepita miezi miwili tangu wakutane,
“Sema ukweli?haki ya mungu ukijifungua mtoto wa kiume nakupa nusu ya utajiri wangu”Aliongea Alex,
“Mipango ya mungu hiyo lakini naamini mungu atasikia kilio chetu” Aliongea Amina na wote wakakumbatiana kwsa furaha.Mama yake Maria alivumilia manyanyaso yam me wake kwani Alex alipolala nje hgakutaka kuulizwa swali lolote,
“Ilimradi mnakula humu ndani sasa kingine nini? Nafanya biashara zangu sitaki kufuatiliwa”Aliongea Alex kwa hasira akimtaka mke wake aliyekuwa na mimba asimfuatilie.Baada ya miezi tisa mkewe alijifungua mtoto mwenyewe ndo Maria,
“Nilijua tu kuwa ndo kama kawaida yako” Aliongea Alex akionyesha kutokufurahishwa na watoto wa kike.Hapo alibaki kumsubiri Amina naye ajifungue kwani alikuwa amebakiza mwezi mmoja.Alex alionyesha kumjali sana Amina kuliko mke wake halali.Hakujua kuwa ile mimba ilikuwa sio yake,Amina alichekea moyoni zaidi aliendelea kuomba usiku na mchana ajifungue mtoto wa kiume ili iwe rahisi sana kuzinasa mali za Alex.Aliikumbuka ahadi ya Alex kuwa atampa nusu ya utajiri wake iwapo atajifungua mtoto wa kiume.Hapo hapo alipiga magoti chini na kuomba ajifungue mtoto wa kiume.Wiki moja mfululizo Alex hakulala ndani alikuwa na Amina hakujali kuwa mke wake naye kajifungua na bado ana maumivu hivyo anahitaji faraja walau kutoka kwa mwanaume.Yote hayo aliyaweka pembeni akili akaihamishia kwa Amina ambaye sasa ilikuwa mda wowote kuwa anaweza kujifungua.Alimhamishia katika hospital ya Mount Meru ili hata akitaka kujifungua basi kusiwepo na shaka yeyote.Bahati nzuri Amina akajifungua mtoto wa kiume ikawa furaha kwa Alex bila kujua kuwa mtoto Yule si damu yake,
“Haya sasa mke wngu mungu kasikia kilio chetu chagua zawadi yeyote mimi nitakupa” Aliongea Alex wakiwa bado hapo hapo hospital,
“Zawadi yangu ni kwamba umuue huyo mwanamke unayeishi naye ili mimi na wewe tuishi kwa raha bila kujificha” Aliongea Amina akimwambia Alex..
kipi kitajiri hapoo?Alex alikubali?hii kwanini inaitwa SITOKUSAHAU? Na je Kwanini Tony anasema kuwa anauchukia umasikini?kuna nini ndani yake? Maria naye kwanini anakuwa na hali ya huzuni kila mda?Usikose sehemu ijayo…