SITOKUSAHAU.
SEHEMU YA-03.
Baada ya Amina kujifungua mtoto wa kiume ikawa furaha kwa Alex ambaye alimhitaji mtoto wa kiume kupita kiasi,hivyo hata mke wake alimuona kama takataka kwani aliamini kuwa Amina ndo atakuwa mke wake.Aliachia tabasamu kuwa kampata mrithi wa mali zake,
“Watoto wa kike hawana maana kabisa unaweza kuwa nao hata kumi lakini wote wataolewa na wewe utabaki peke yako.Hongera mpenzi wangu kwa kunizalia dume hakika ntakupenda na kukujali daima” Aliongea Alex huku akiwa amemkumbatia Amina,
“Sasa ombi langu?maana sina amani kabisa huyo mke wako anaweza kuniwahi akaniua.Naogopa kumuacha Bahati wangu pamoja na wewe”Aliongea Amina.Mtoto wake alimuita Bahati akiamini kuwa atakuwa na bahati ya kurithi mali ilihali sio za baba yake,
“Oooh la kumuua Yule kinyago?”Aliuliza Alex huku mke wake wa ndoa akimuita kinyago,
“Ndio mme wangu nataka tuishi kwa amani mpenzi wangu”Alijibu Amina kwa kudeka na bila kutarajia Alex akakubali ombi lake kuwa asijali mkewe atauawa.Amina alifurahi na kumpiga busu la shavuni Alex.Siku zilisogea,Alex akazidi kubadilika kila kukicha,alilala nje mwezi mzima.Hata alipokuwa anakuja nyumbani hakutaka kuulizwa na mkewe hivyo alifanya anachokitaka.Mkewe al;ikuwa na mtoto wa miezi mitatu tu na ndo Yule Maria,alivumilia manyanyaso,akavumilia kila kitu.Siku moja Alex alirudi nyumbani akiwa amelewa,alifika ndani na kuanza kufoka,
“Yaani wewe mwanamke nakuchukia sana kila kuzaa basi ni matoto ya kike tu,kwa taarifa yako mimi tayari nina mtoto wa kiume ambaye atakuja kurithi mali zangu” Aliongea kwa sauti ya kilevi Alex huku akitoa simu yake na kumpigia Amina lengo amuumize mkewe,
“Yeaah mama bahati nimekuja huku kuchukua hela nakuja hapo nikute unaendelea kunywa”Alex aliongea kwa sauti,
“Wahi babay jamani nina baridi nahitaji joto lako”Sauti ya upande wa pili ilisikika ambayo ilikuwa ni ya Amina.Maneno yale yakawa mkuki moyoni mwa mama yake Maria,akaumia kupita kawaida.Alex kutoka na pombe alizokuwa amekunywa alilala na usingizi ukampitia,mkewe akachukua simu na kuangalia ujumbe waliokuwa wanatumiana na Yule mwanamke.Alishtuka baada ya kuona kuwa Alex anatembea na mtoto wa mama yake wa kambo.Yaani Amina na mama Maria walizaliwa na baba mmoja ila mama tofauti.Roho ilimuuma kuwa kikulacho kinguoni mwako.Kingine kilichomshtua zaidi ni pale aliposoma ujumbe ulioonekana kutumwa siku nne zilizopita,
“Fanya mpango huyo kinyago afe ili tuishi kwa amani mimi na wewe” Ujumbe ule ulisomeka hivyo
“yaani Amina ndo anataka kuniua mimi?kwa kosa gani?”Alijiuliza mkewe Alex na ndipo akakumbuka tangu utotoni Amina alikuwa hampendi,
“Hapa ni kukumbia kabla maafa hayajanikuta”Alijisemea na tangu siku hiyo akawa makini sana kusudi asiuawe.Baada ya mwaka mmoja kupita ndipo akapanga kutoroka kweli alifanikiwa akawaaga watoto wake wote ambao walikuwa wameolewa tayari.Akakimbilia jijini Mbeya.Hata hivyo Alex hakuacha kumfuatilia.Miaka mitatu akipita ndipo Alex akawatuma watu wa kwenda kumuua huyo mwanamke kisha warudi na Maria pekee,kweli walifanikiwa kwa wakati ule Tayari Alex alikuwa anaishi na Amina.Tangu siku ile Maria akawa chini ya Amina,alinyanyasika hata kunyimwa chakula.Licha ya kuwa na miaka mitano kwa wakati ule lakini tukio lililotokea alipanga kulipa kisasi kwa badae.Akiwa na miaka mitano alipelekwa shuleni lakini bado manyanyaso yalikuwa yale yale kutoka kwa mama wake wa kambo.Hakuwahi kutabasamu hata siku moja,dada zake waliokuwa wameolewa hakuna aliyedhubutu kuishi naye wakamuacha.Maria aliona dunia kama vile imemtenga na kujiona hana thamani tena dunian i.Lakini alijipa moyo kuwa hakuna lenye mwanzo alafu likose mwisho.Alijipa imani kuwa ipo siku yatakwisha,akavumilia kula kwa shida na kulala kwa taabu.Bado moyoni alikuwa na kisasi kizito kwa Amina na alipanga kulipiza mda usiojulikana.Darasa la saba likamalizika ndipo akaingia shule ya sekondari.Kwa wakati huo Bahati naye alikuwa anaingia sekondari lakini kichwani mwake hakuwa na akili hata kidogo.Alikuwa shule ile ile ya St James ambayo alisomea pia Tony.Hata hapo mambo yalikuwa yale yale mara nyingi alivuka darasa kwa nguvu ya pesa tu ambayo baba yake alihonga walimu pia na wasimamizi wa mitihani.Siku zikasogea na ndipo wote wakamaliza shule za sekondari huku Tony akiacha rekodi shuleni pale ya kuwa mwanafunzi bora aliyetisha kwenye masomo ya sayansi,kila mwalimu alitamani Tony asimalize shule abaki pale pale kwani alikuwa mwanafunzi asiye na makuu hata kidogo,mda mwingi alimkosoa hadi mwalimu pale alipokosea.Lilipokuwa linakuja somo la hesabu hilo alilipenda sana hivyo mama yake kijijini aliuza shamba akiwa na matumani kuwa lazima mwanaye afike mbali sana lakini mwisho wa yote matokeo yakaja kuwa Tony hajachaguliwa kuendelea na kidato cha sita badala yake atafute chuo kwani matokeo yake hayakuridhisha.Kila mmoja alishangaa,
“Tony huyu huyu ninaye mjua?hapana hapa kuna kitu”Alijisemea mwanafunzi mmoja aliyekuwa rafiki wa Tony na alimpa asilimia zote kuwa lazima Tony angechaguliwa kuendelea na kidato cha sita.
*
Hivyo Maria kuwa mpweke pale chuoni kuna jambo zito linamsumbua na anahitaji kulipa kisasi ili moyo wake utulie na uwe na amani kabisa.Bado moyo wa Tony ulimpenda Maria lakini akajitahi kuzuia hisia zake huku maneno ya mama yake yakijirudia rudia kichwani.Akazidisha bidii huku mara nyingi kwenye madaftari yake akiandika maneno kuwa “NAUCHUKIA UMASKINI”Hakuna aliyejua lengo la kuandika vile kutokana na Tony kuwa bize shuleni pale na hakutaka kuongea na mtu.Aliwachukia watoto wa matajiri kupita kiasi.Alitamani dunia yote igeuke na kila mmoja awe maskini yaani kusiwepo matajiri binadamu wote tuwe sawa ili asinynyasike mtu yeyote,
“Kumbe ndo maana maneno ya mungu yanasema kuwa ni rahisi ng’amia kupita kwenye tundu la sindano ila sio rahisi tajiri kuingia mbinguni” Alijisemea Tony.Matajiri wote aliona ni wana wa shetani na sio wa mungu tena.Aliendelea kujisomea kwa juhudi ili aone kama ataweza kuondokana na umasikini,
“Hata nikipata hela za kujaza dunia nzima siwezi kuwa nyanyasa maskini”Alijisemea Tony.Siku ile alionekana mwenye mawazo sana,alikumbuka mbali sana,alitamini sana kuwa daktari ndo maana aliyapenda masomo ya sanyansi na kweli alimudu vyema.Kila alipokuwa anakumbuka hicho machozi yalimtoka kwa wingi lakini aliyafuta na kujisemea kuwa nafasi bado ipo lakini kitendo kile kilimrudisha nyuma alitamani kujipanga upya na kusimama tena kwa mara nyingine.Hakuna aliyejua siri iliyokuwa moyoni mwake si mjuomba wake wala mama yake.Aliijua yeye mwenyewe na alitamani kulipa kisasi si kwa ubaya bali kisasi kitakachoweka mambo yote hadharani,
“Ipo siku kila kitu kitakuwa wazi huenda hata viongozi wa ngazi za juu wakanitetea”Alijisemea Tony.Hisia za mapenzi hazikuwa kwa Tony tu bali hata kwa Maria naye alimpenda Tony,alijitahidi kuvumilia lakini ilishindikana akaamua kuziweka wazi.Mda mwingi akawa anajipeleka kwa Tony huku akidanganya kuwa amekuja ili amsaidie walau mambo ya masomo.Mwili wa Maria ulipokuwa unagusana na wa Tony Maria alijihisi raha ya ajabu sana.Wanachuo wasiopenda kuongea basi walikuwa wamekutana watu wengi walicheka sana kuwa kipofu kwa kipofu wameshikana.Siku zikakatika huku urafiki wa Tony na Maria ukizidi kukua kila kukicha.Mwanzo ulionekana urafiki wa kaida kumbe ndani yake kuna kitu..
Bado tuko gizani,kuna nini katikati?Tony kwanini anawachukia matajiri wote?Kisasi cha Maria kitatimia?Maria kashikana na Tony.Wote wana visasi vizito..NAKUSIHI TU ENDELEA KUWA NAMIMI MWANZO MWISHO..