;
SITOKUSAHAU. sehemu ya-04. | Mahusiano Yetu

Type something and hit enter

By On

 SITOKUSAHAU.


sehemu ya-04.

Amiboy x Japhee - Sitokusahau. (Official audio) - YouTube

Kadri siku zilivyokuwa zinasogea ndivyo urafiki wa Maria na Tony ukazidi kukua kwa kiasi kikubwa.Walikuwa wote kila sehemu ile tabia yao ya kukaa ndani ikawaishia kabisa,kila mmoja akawa anamsifu mwenzake kwa kumuondolea hali ya upweke.Siku zikasogea huku kila mmoja akionekana kuwa na kitu cha kuongea lakini ikawa shida,kila mmoja alionekana kuwa na aibu kupita kawaida.Ilikuwa siku ya juma tatu siku hiyo Maria aliipania na alipanga kumweleza ukweli Tony,

“Ya nini kuutesa moyo wangu ilihali uwezo wa kuongea ninao?acha nikauvunje ukimya”Alijisemea Maria huku akiwa anazipiga hatua kuelekea chuoni.Hata alipofika akamuona Tony,hakusita  alimuita na Tony akatii wito.Siku hiyo Maria alionekana kuwa na jambo zito la kuongea,

“Samahani sana Tony,ila ukweli ni kwamba nakupenda sana nimerjizuia nimeshindwa tafadhali naomba usikie maneno yangu na uamini kuwa hisia ndo zimenituma mimi kusema haya”Aliongea Mariamara bada ya salamu.Tony alimeza funda moja la mate licha ya kuwa alitambua tangu awali kuwa Maria anateseka juu yake,hata kwa upande wake naye kuna mda alikuwa anateseka lakini kila alipoyakumbuka maneno ya mama yake basi alijitahidi kujizuia,

“Ahsante sana Maria kwa kunipenda”Alijibu Tony,

“Ahsante nini Tony?ina maana hujali kilio changu?”Aliongea Maria huku taratibu machozi yakimlenga lenga.Tony alikaa kimya kwa mda akionekana kutafakari kitu,

“Sawa natambua vyema kuwa wanipenda lakini mimi mama yangu kanizuia kujiingiza kwenye haya mambo”Aliongea Tony,

“Sasa mama kama amekuzuia sio shida huenda kataka usipotee ili badae uje upate mtu aliyesahihi kwa upande wako na ndo mimi hakuna mwingine”Aliongea Maria kwa hisia kali.Tony hakuwa na ujanja wa kukataa akajikuta anamkubalia Maria na huo ndo ukawa mwanzo wa mahusiano yao.Mahusiano yaliyoanza kwa nguvu huku kila mmoja akitamani kuwa na mwewnzake kila mda.Kwa siku chache karibia wanachuo wote waliyajua mahusiano yao,licha ya Maria kuwa mpole lakini kwa Tony alionekana mchangamfu sana.Bado Tony maneno ya mama yake aliyakumbuka vyema lakini aliamini kuwa Maria ni mtu sahihi kwake.Siku zikakatika,sasa walikuwa wameaminiana ndipo kila mmoja akaanza kumsimlia mwenzake yalito moyoni mwake,

“Umeona sasa huyu mama wa kambo ndiye aliyemshawishi baba kumuua mama yangu,yaani nina kisasi naye naamini kitatimia tu”Aliongea Maria akionyesha kumchukia mama yake wa kambo ambaye ni Amina.Alielezea kila kitu jinsi alivyonyanyaswa tangu mama yake apoteze maisha,

“Mama yangu hakuwa muongeaji sana wala hakuwa na visa na mtu lakini wamemuua.Siwezi kumlaumu baba yangu najua ni huyu mama wa kambo alimsawishi.Mungu amlaze mahali pema”Aliongea Maria huku akiinua mikono yake juu ishara ya kumuomba Mungu ili mama yake apumzike kwa amani kwani hakuwa na kosa lolote lile.Aliuawa tu kwa tama za Amina za kutaka kuwa mke halali wa Alex,

“Pole sana kumbe ndo maana ulikuwa kimya mda wote una mambo mazito”Aliongea Tony,

“Ndio ila lazima nitalipa kisasi hata ikiwa miaka miambili naamini kisasi kilichoko moyoni mwangu kitatimia”Aliongea Maria huku akiyafuta machozi yaliyokuwa yanamtoka.Tony alimfariji licha ya kuwa yeye hakutaka kuelezea kilichokuwa moyoni mwake,

“Eeeh na wewe naona mda mwingi upo kimya kipi kinakusibu?”Aliuliza Maria,

“Hapana mimi lango lilikuwa ni kwenda kidato cha sita lakini nilifeli ndo maana nakuwa mpweke sana”Aliongea Tony akijaribu kuuficha ukweli,

“Pole sana hata hivyo hii nafasi uliyopo sio mbaya sana”Aliongea Maria.Tony aliitikia kwa kichwa,

“Umesema baba yako ndo anaitwa nani?”Aliuliza Tony,

“Baba yangu anaitwa Alex ndo Yule mwenye magari ya abiria yaliyoandikwa Alex Trans”Aliongea Maria.Tony kusikia jina hilo akashtuka sana,mapigo ya moyo wake yakaenda mbio sana,jasho likampanga na kuilegeza tai yake iliyokuwa shingoni mwake,akamgeukia tena Maria akamtazama mara mbili na kuona kweli Maria anafanana na baba yake,sekunde kadhaa zikapita Tony akiwa bado na hali ile ile,lakini badae akawa kawaida japo machoni mwake alionekana kutokuwa sawa kabisa,

“Mbona umeshtuka hivyo wanguy kuna ninini?”Aliuliza Maria alipomuona Tony akiwa na hali tofauti,

“No”(hapana) niko kawaida sema nawaza jinsi gani baba yako alivyo tajiri mkubwa hapa Moshi lakini kashindwa kukusomesha shule za gharama kuliko hii?hawa wazazi ndo wanatuharibu wenyewe wakati wanatambua kuwa elimu inatafutwa”Aliongea Tony kwa masikitiko makubwa.Alivuta picha Alex jinsi alivyo tajiri mkubwa lakini kwa upnde wa Tony aliwachukia matajiri wote akiwemo Alex.Hivyo kitendo cha kujenga mahusiano na Maria aliona kama vile yuko karibu na adui yake na tangu siku hiyo Tony akakatisha mahusiano na Maria,akawa peke yake hakutaka kumuona hata Maria mbele yake.Maria akawa mnyonge sana,hakujua kilichombadilisha Tony hadi kuwa kwenye hali kama ile,alijaribu kumchunguza akidhani labda Tony kapata mwingine lakini ukweli ukabaki pale pale kuwa Tony  hana mtu yeyote.Kipi kimembadilisha sasa? Lilikuwa swali la Maria kichwani mwake,

“Au kwakuwa sijampa penzi langu ndo maana? Lakini hapana hajawahi kuniambia hayo maneno”Alijisemea Maria lakini bado hakujua kilichokuwa moyoni mwa Tony.Hakukuwa na kosa lolote alilomkosea kitendo cha kusema baba yake ni Alex ndo kilichomfanya Tony avunje uhusiano wao.Moyoni Maria aliumia sana,hakuwa tayari kuona mtu anayempenda kama Tony anatengana naye,chuoni alipaona hapakaliki,akatamani kuingia moyoni kwa Tony ili atazame kilichokuwa moyoni mwake.Maria akawa mtu wa kujiinamia mda wote.Kila mara Tony alionekana kutazama paa la nyumba na hiyo yote ni mawazo.Alinyanyuka na kwenda kuandika ubaoni,

“NAUCHUKIA UMASKINI PIA NAWACHUKIA MATAJIRI WOTE”Maneno yale ya Tony yalizua mjadara kila mmoja akisema lake,

“Ni kweli kabisa matajiri waliowengi wanawanyanyasa maskini”

“Wewe unaongea nini?kwa hiyo unataka duniani wote tuwe sawa je nani atamfanyia kazi mwenzake?”

“Yeah ila amini kuwa matajiri wote hakuna atakayeenda mbinguni”

“Bora uukose utajiri wa duniani uupate wa mbinguni maana huo utakuwa ni milele,lakini wa hapa duniani utakufa na utauacha” Yalikuwa ni maneno ya wanachuo wakionekana kuijadili mada ya Tony aliyoiandika ubaoni kila mmoja alisema lake.Kila mwanachuo alimuuliza Tony kuwa kwanini anauchukia umaskini? Kwa sababu kila kukica Tony alikuwa anayaongea hayo maneno,

“Kwa sababu mimi ningelikuwa tajiri nisengelikuwa hapa,ila yote kwa yote namshukuru Mungu  tu”Aliongea Tony maneno yaliyowaacha vinywa wazi wanachuo.Hiyo ndo ilikuwa mara yake ya kwanza Tony kuongea,mda mwingi alikuwa kimya,kila mwanachuo akajiuliza leo imekuwaje hadi Tony akaongea?.Siku zikasogea huku Tony akimuondoa Maria moyoni mwake,

“Siku zote bwana moyo unasukuma damu na si mapenzi”Alijisemea Tony pale alipojaribu kumfikiria Maria.

*

Uvumilivu ukamshinda Maria akaamua kumfuata Tony ili walau amuulize tatizo lililomfanya yeye kuwa kwenye hali kama ile,

“Sina tatizo ila nimeamua tu kuwa masomo kwanza mapenzi badae”Aliongea Tony,

“Hapana unaposema hivyo unakosea,sasa mapenzi yanakuzuia usisome?mimi nakupenda sana niko tayari kwa lolote pia nakuhaidi kuwa sitokusumbua labda wewe ukipata mda”Aliongea Maria kwa sauti ya chini iliyojaa simanzi.Wanawake wakipenda wamependa kweli,

“Tatizo sio hilo”Aliongea Tony,

“Ila tatizo nini?”Nambie Tony ili nijue  naumia sana Tony unapokuwa kwenye hali kama hiyo,

“Baba yako ni mnyama pia ni shetani asiyefaa kuishi kwenye hii dunia”Aliongea Tony na maneno yale yakamuacha kinywa wazi Maria,

“Baba?baba yangu kafanyeje?”Aliuliza Maria kwa mshangao,

“Kiufupi namchukia baba yako hata na wewe pia nakuchukia.Nasema tena baba tako ni nyoka na siku zote ukiishi na nyoka nadhani madhara yake unayajua”Aliongea Tony kisha akaondoka akimuacha Maria ameduwaa…

Kwanini Tony kasema vile?ana siri gani moyoni mwake?je,hiyo siri ataisema kwa Maria?aseee kuna mengi sana kwenye hi simulizi,Baki  namimi….

Pata Ajira ya ndoto yako leo BONYEZA HAPA ili kuperuzi Nafasi za kazi Zinazotangazwa kila siku DOWNLOAD/INSTALL Ajiraforum App zisikupite