;
SITOKUSAHAU. Sehemu ya-05. | Mahusiano Yetu

Type something and hit enter

By On

 SITOKUSAHAU.



Sehemu ya-05.

Amiboy x Japhee - Sitokusahau. (Official audio) - YouTube

Maria alijiuliza maneno aliyoambiwa na Tony lakini hakuyaelewa,alibaki kuumia na kuona kama vile Tony kamtukana baba yake.Hakujua kwanini Tony katamka maneno yale kuwa baba yake ni zaidi ya nyoka kwa mabaya aliyomfanyia,

“Hapana lhapa lazima nimuuulize kwanik baba yangu kafanya nini?”Alijiuliza Maria lakini jibu hakulipata.Tony alikatisha mahusiano na kumtaka Maria asimsumbue tena,

“Sasa Tony ubaya kama ulifanyiwa na baba mimi nahusika vipi tena?hujui kuwa naumia kwa unayonifanyia?”Aliongea Maria kwa sauti iliyojaa majonzi kwani moyo wake ulikuwa tayari umempenda Tony.Licha ya kusema vile lakini Tony hakuongea chochote,ilibaki siri yake moyoni,

“Ipo siku ukweli utajulikana tu”Aliongea Tony na kuondoka.Maumivu ya mapenzi yakamjaa Maria akatamani kurudi nyumbani siku ile ile ili akamuulize baba yake kitendo gani alimfanyia Tony,

“Ngoja wiki hii lazima niende nyumbani nikamuulize baba”Alijisemea Maria na kujitahidi kuuzuia moyo wake uyazoee yale maumivu lakini ilikuwa ngumu,maumivu ya mapenzi huwezi kuyavumilia,alishindwa na kujikuta tena akitamani kuongea na Tony.Njia za kuongea na Tony hakuwa nazo tena akabaki akiwa mnyonge kama kinda alokosa mama.

*

Kitu ambacho Alex alihakikisha kuwa kinafanyika basi ni hili la mtoto wake Bahati,alitamani Bahati awe na akili nyingi kuliko mtu yeyote Yule katika shule aliyokuwa anasomea kidato cha sita.Alijitahidi kumtafutia mwanaye shule zilizo bora pia zilizosifika kwa kufauru matokeo.Akapata shule moja inayoitwa Tosamaganga iliyoko Iringa,hiyo akaiamini kuwa huenda itamfaurisha mwanaye.Pamoja na kufanya hayo yote lakini mwanaye hazikuwemo kabisa,alishika nafasi za mwishoni katika shule ili.Kila mmoja aliamini kuwa Bahati kapita kwa nguvu za pesa na si kingine,hakuelewa hata kidogo,walimu wenye viwango vya juu walijitahidi kumfundisha na kumuelekeza mambo mengi lakini bado hakuelewa chochote.Alex aliumia lakini hakukata tama ya kumsomesha mwanaye,aliamini kuwa ni mwanaye kwa asilimia moja lakini siri ilibaki kwa Amina ambaye ni mke wake kwa wakati ule.Elimu bora akaitafuta kusudi mwanaye aipate ili badae arithi utajiri wake ulionekana kukua kwa kasi ya ajabu,kila kukicha aliongeza maduka pamoja na kujenga nyumba pale Moshi mjini.Alex alikuwa na utajiri mkubwa sana lakini licha ya kuwa vile hjakuwahi kumsaidia mtu yeyote,wengi wao aliishia kuwafanyisha kazi ngumu na kuwalipa ujira kidogo,wengi wao aliwadhurumu kabisa.Lawama nyingi kutoka kwa wanakijiji alizipokea pale mifugo yake kilipokuwa inaharibu mashamba ya watu,

“Dua la kuku halimpati mwewe”Ndo maneno aliyoyatumia pale wnakijiji walipokuwa wanamlaumu.Bado hakupata mtoto mwingine tangu aoane na Amina na kumuua mke wake halali,

“Mke wangu nataka mtoto mwingine”Aliongea Alex akiwa na Amina.

“MMme wangu mtoto atakayerithi mali zako yupo kwahiyo usiwaze Mungu atatujalia tutapata tu mwingine”Aliongea Amina na kujaribu kumtia moyo  Alex ili ikiwezekana kwa badae amuue kisha mwanaye Yule arithi mali zake zile bila shida.Hiyo ipo kwa wanawake wengi,akimuona mme wake kafanikiwa basi anamuua ili utajiri ule uwe mikononi mwake.

*

Kitendo cha Tony kumnyima furaha Maria kilimuumiza sana,alitamani kujua kitu kilichoko moyoni mwa Tony lakini bado Tony hakutaka kusema lolote.Ikiwa ni jioni wanachuo wengi walikuwa mazoezini huku wengine wakiwa wamekaa makundi makundi wakiopnekana kujadili mada tofauti tofauti.Maria likuwa chini ya mti akionekana mwenye mawazo sana.Badae alijikongoja na kuzunguka nyuma ya jengo moja lililopo chuoni hapo ambapo huko alimkuta Tony naye akiwa peke yake,alizipiga hatua fupifupi akamfuata,alipomfikia akaketi chini,

“Habari yako Tony’Alisalimia Maria na Tony akaitikia.Mara baada ya kujibu salamu ile akainuka kutaka kuondoka lakini Maria akamshika mkono,

“Tony kama hauko tayari kuniambia kile alichokufanyia baba yangu basi mimi kesho naenda kumuuliza”Aliongea Maria.Maneno yale yakamshtua Tony,hakutaka kile alichonacho moyoni kimfikie Alex ambaye mpaka sasa anahisi jambo alilolifanya halijulikani,

“Hapana usimuulize nitakwambia mimi mwenyewe”Aliongea Tony,

“Haya sasa nambie”Aliongea Maria huku akikazia pale pale,

“Nitakwambia lakini nihaidi kama utaitunza siri hii,maana sitaki my yeyote ajue hata aba yako sitaki ajue”Aliongea Tony,lakini Maria akamuondoa wasiwasi kuwa asiwe na shaka hakuna atakachokisema.Tony akameza funda moja la mate,kisha akainua uso wake kumtazama Maria.Kwa uchungu aliokuwa nao akajikuta anadondosha chozi,ambalo alilifuta kwa mkono wake wa kushoto,

“We acha tu,najiuliza kwanini Mwenyezi Mungu hakutuumba binadamu wote tukawa sawa?lakini sitaki kuingilia kazi yake.Ukweli ni kwamba mimi nyumbani kwetu maisha ni magumu sana.Kuna mda tunashindia tu mlo mmoja lakini yote hayo tunamshukuru mungu bado tunapumua.Mimi ni mtoto wa kwanza kwenye familia yetu,tumezaliwa watatu tu huko kijijini Mngeta kilicho Morogolo.Baba yangu alipoteza maisha na kutuacha tukiwa wadogo sana mimi na wadogo zangu,hali duni ya kimaisha ikanifanya niongeze juhudi kwenye masomo,uweli usiopingika watoto wa matajiri huwa hawajitumi sana kwani wanajiona kuwa haina haja ya kuongeza bidii ilihali utajiri upo kwa wazazi wao.Naweza kusema kuwa mimi mpaka sasa natamani sana kuikomboa familia yangu iondokane na huu umasikini.Matajiri wanawanyanyasa sana maskini jambo hili linaniumiza mno”Aliongea Tony kwa uchungu mpaka machozi yakamtoka.Akatafuta kisha akaendelea,

“Baba yako ni mtu wa kwanza ambaye namchukia kwenye hii dunia.Baba yangu alipopoteza maisha nikahamia huku Moshi na mpaka sasa naishi kwa mjomba ambaye ananijali sana.Shamba ambalo lingewasaidia hata wadogo zangu limeuzwa tayari kwa ajili yangu.Niliyaanza masomo ya sekondari nilisoma kw bidii sana,darasani kwetu nilikuwa nashika namba moja au mbili lakini sikuwhi kushika namba sita kwenda juu.Nilipendwa sana na walimu kutokana na juhudi zangu binafsi,masomo ya sayansi niliyapenda kupita kawaida na kweli yakaniingia kichwani.Kila mda nikawa nashinda maabara nikifanya majaribio mbali mbali na baadhi ya walimu pamoja na wanafunzi wachache waliokuwa na uwezo kama wangu.Nikiwa kidato cha pili nilishika nafasi ya tatu kimkoa,wengi walinitazama kwa jicho la tatu kuwa sisitahili kusomea shule kama hizi kwa maana uwezo wangu ulikuwa mkubwa nilitakiwa kupelekwa hata shule za nje ya nchi au zenye hadhi kubwa lakini yote hayo naulaani umaskini.Kidato cha tatu nikasoma kwa bidii zaidi,nikawa natesa pale shuleni.Shule nzima ya St James ikalifahamu jina langu pamoja na uwezo wangu mkubwa,hakika nilijivunia hilo.Sikutaka kulewa sifa hata kidogo kila kukicha nikawa natamani kujua mengi zaidi.Yalipotokea mashindano ya kuongea kingereza na shule jirani niliitwa nikiwa wa kwanza.Watu walinipenda kutokana na upole wangu na kutokujionyesha kwa watu kama watu wengine jinsi walivyo ambao wanajiona kuwa wamefanikiwa.Kidato cha tatu kikamalizika,tukaingia cha nne,hapo sasa ndo nikazidisha juhudi kwani hiyo ndo ilikuwa fainal,sikutaka kulala usiku kucha nilikesha nikijisomea.Mtihani ukawadia kutokana na kujifunza mambo mengi mtihani ulikuwa mwepesi sana na nilitegemea  kushika nafasi za juu,sio mimi tu hata walimu matumaini waliyaweka kwangu na kila mmoja aliniambia kuwa nitegemee ufauru wa hali ya juu.Moyoni nikawa na furaha,nikiwa kweenye chumba cha mtihani kuna maswali kadhaa niliyakariri hivyo mtihani ulipokwisha nikawa nayafanya kila mtu akanisifia.Ninaposema namchukia baba yako na maana kuwa baba yako ndo aliyanunua matokeo yangu na kumpa mwanaye mimi nikaonekana nimefeli kwa kiwango kikubwa sana,walimu hawakuumia zaidi maana walikijua kile kilichofanyika.Wanafunzi wengi walinisikitikia mwanzoni sikujua lakini badae nikajua kuwa baba yako baada ya kuniona mimi maskini akaamua kufanya vile.Lazima nilipe kisasi,namchukia sana baba yako namuona ni mtu asiyefaa hata kuishi kwenye hii dunia.Kwanini alikatisha ndoto zangu?kisa yeye tajiri?nasema hivi namchukia pia hata wewe nakuchukia”Aliongea Tony kwa uchungu na kumsukuma Maria akionyesha naye pia anamchukia na anahitaji kulipa kisasi…

Hatimaye tumekipata kilichokuwa kinamsumbua Tony,ni kipi kitatokea hapo katika sehemu ya sita?Tony anataka kulipa kisasi gani?kwanini hii inaitwa SITOKUSAHAU? Kuna mengi sana ya kujifunza kwenye hii simulizi,Tukutane sehemu ijayo……

Pata Ajira ya ndoto yako leo BONYEZA HAPA ili kuperuzi Nafasi za kazi Zinazotangazwa kila siku DOWNLOAD/INSTALL Ajiraforum App zisikupite